August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taifa Stars yabanwa mbavu nyumbani

Wachezaji wa Taifa Stars ikimlinda mchezaji wa Rwanda katika mchezo huo

Spread the love

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindwa kutamba katika uwanja wa nyumbani baada ya kukubali sare ya bao 1-1 dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’ katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, anaandika Erasto Masalu.

Amavubi ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 17 kupitia kwa Domicique Nshuti dakika ya 18 kabla ya Himid Mao kuisawazishia Taifa Stars dakika ya 34 kwa mkwaju wa penalti.

Matokeo hayo yanaipa wakati mgumu Taifa Stars, kwani inatakiwa kushinda katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumamosi ijayo jijini Kigali Rwanda.

Taifa Stars ikifanikia kushinda katika mchezo huo wa marudiano itasonga mbele katika hatua nyingine ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) zitakazofanyika Kenya mwakani.

error: Content is protected !!