January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taifa Stars yaanza vibaya COSAFA

Mshambuliaji wa Taifa Stars, Siomn Msuva akimtoka beki wa Swaziland

Spread the love

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeanza vibaya michuano ya Kombe la COSAFA, baada ya kukukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Swaziland katika mchezo wa kwanza wa Kundi B, uliopigwa kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace, jijini Rustenburg, Afrika Kusini.

Bao lililoizamisha Taifa Stars lilifungwa dakika ya 42 ya mchezo huo kupitia kwa Sifiso Mabila akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Xolani Sibandze aliyemtoka Oscar Joshua.

Kwa matokeo hayo Taifa Stars imekuwa katika wakati mgumu wa kupenya katika hatua ya robo fainali, baada ya matokeo ya mchezo wa kwanza baada ya Madagascar kuifunga 2-1 Lesotho.

Stars italazimika kushinde mechi zake mbili zijazo dhidi ya Lesotho na Madagascar ili kuangalia uwezekano wa kwenda Robo Fainali.

error: Content is protected !!