June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taifa Stars yaaga CHAN, yalazimishwa sare Uganda

Kikosi cha Stars kilichoanza leo dhidi ya Uganda

Spread the love

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeaga michuano ya CHAN baada ya kutoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda ‘The Cranes’ katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017 nchini Rwanda uliofanyika uwanja wa Nakivubo.

Kwa matokeo hayo, Uganda imesonga mbele katika michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani kwa jumla ya mabao 4-1, kutokana na ushindi wa mabao 3-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Zanzibar wiki mbili zilizopita.

Stars ambayo leo imeonekana kabadilika katika mchezo wa leo, ilicheza soka la kuvutia tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaduwaza wenyeji Uganda.

Mpaka dakika 45 za mchezo za kipindi cha kwanza zinamalizika, Uganda 0 – 0 Tanzania. Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi mfululizo kupitia kwa washambuliaji wake John bocco na Rashid Mandawa.

Dakika ya 58, John Bocco aliipatia Tanzania bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti kufuatia mlinzi wa Uganda Bakaki Shafik kuunawa mpira wa ndani ya eneo la hatari.

Mara baada ya bao hilo Uganda walifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Stars na kufanikiwa kupata bao la kusawzisha dakika ya 82, kupitia kwa mchezaji Kizito Hezron.

Mara baada ya mchezo huo kochaa mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema anashukuru vijana wake wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo ulikua mzuri timu ilitengeneza nafasi chache na kuweza kutumia nafasi moja iliyopatikana.

Mkwasa amewaomba Watanzania kuendelea kuwapa sapoti, wamekaa na timu kwa muda mfupi wa wiki moja tu lakini katika mchezo wa leo mabadiliko yameonekana, hivyo wanahitaji muda kidogo kuweza kukaa na vijana kwa muda mrefu ili kujenga timu bora.

Stars inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda Air.

error: Content is protected !!