November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Taifa Stars kutupa karata muhimu kuelekea Kombe la Dunia 2022

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kikiwa mazoezini

Spread the love

TIMU ya soka ya Tanzania “Taifa Stars” inashuka katika dimba lake la nyumbani la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuwakabili DR Congo, kuwania kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni leo Alhamisi, tarehe 11 Novemba 2021 kuanzia saa 10:00 jioni.

Stars inayoongoza kundi J ikiwa na pointi saba sawa na Benin lakini ikiwa na uwiano mzuri wa magoli ya kufungwa na kufunga, itashuka tena dimba hilohilo, tarehe 14 Novemba 2021, kuwakabili Madagascar.

Katika kundi hilo, Congo inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tano huku Madagascar ikishika mkia ikiwa na pointi tatu.

Mchezo mwingine wa kundi hilo, utapigwa leo kuanzia saa 1:00 usiku, Benin itakapowakalibisha Madagascar.

Aidha, Serikali ya Tanzania chini ya Waziri Mkuu wake, Kassim Majaliwa kwa nyakati tofauti aliitembelea Stars kwenye uwanja wa mazoezi na kambini na kuzungumza nao.

Majaliwa alikutana na wadau wa soka nchini humo na kuchangisha Sh.1.6 bilioni ili kutoa hamasa kwa kambi hiyo katika michezo yote ili kuhakikisha inafuzu michuano hiyo mikubwa ya dunia itakayopigwa Qatar mwakani.

error: Content is protected !!