February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Taifa Stars kutua Cape Verde na Dreamliner

ATCL Dreamliner

Spread the love

TIMU ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars itatua jijini Praia, nchini Cape verde na Dreamliner mali ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuvaana na wenyeji hao kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuvu kwenye fainali za kombe la matifa huru ya Afrika (AFCON) unaotarajia kuchezwa 12 Octoba 2018. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Akiongea mbele ya waandishi wa habari leo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe alisema ndege ya hiyo ambayo itabeba wachezaji pamoja na mashabiki 200 itarejea nchini mara baada ya mchezo huo kumalizika ili kuwahi kujiandaa na mchezo wa marudiano utakaochezwa 16 Octoba, 2018 jijini Dar es Salaam.

“Kitendo cha timu kushuka Cape Verde na Dreamliner, tena ndege ya nyumbani, tayari tumekwishawapiga goli mbili, hizo goli nyingine namuachia Amunike na benchi la ufundi waongezee,” amesema Waziri Mwakyembe.

Waziri huyo aliongezea kuwa kutokana na ndege hiyo kuchukua watu 200 huku wakati msafara mzima wa Taifa Stars utakuwa na watu 31, hivyo kutakuwa na nafasi kwa mashabiki watakaopenda kusafiri na timu hiyo itawalazimu kuchangia dola za kimarekani 1,500 sawa na S. 3.5 milioni kwa tiketi ya kwenda na kurudi.

“Wachezaji na viongozi watakaokwenda Cape Verde hawatazidi 31, Dreamliner ina uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 200, hivyo tunaomba mashabiki wajitahidi kununua tiketi tukaishabikie timu yetu ya taifa,”

Stars watakuwa wagenini kwenye mchezo huo wa kundi L, ambalo linajumuisha timu za Uganda ambaye ndio kinara wa kundi hili akifuatiwa na Cape Verde wanashika nafasi ya pili huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu ikiwa na alama mbili na Lesotho akiburuza mkia.

error: Content is protected !!