TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaingia kambini hii leo kwa ajili ya kujiandaa na michezo miwili ya kirafikia pamoja na mchezo wa kufuzu kwa michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Equatorial Guinea. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Wachezaji walioitwa wataanza kuingia kambini hii leo jioni kwenye hotel ya Tiffany Diamond iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen aliita wachezaji 43, ambao watasafiri kuelekea nchini Kenya kwa ajili ya kucheza michezo miwili ya kirafiki tarehe 16 na 18 Machi 2021, na kisha tarehe 19 kikosi hiko kitasafiri kueleke Guinea kwa ajili ya mchezo wa kufuzu AFCON.
Mchezo huo dhidi ya Equatorial Guinea utapigwa siku ya tarehe 25 Machi, 2021.
Taifa Stars ipo Kundi J inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne, huku ikiwa imebakisha michezo miwili ambayo inahitaji ushindi ili iweze kufuzu.
Vinara wa kundi hilo mpaka sasa ni Tunisia akiwa na pointi 10, ikifuatiwa na Equatorial Guinea kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi sita, nafasi ya tatu Taifa Stars ikiwa na pointi nne, huku Libya ikiwa mkiani wakiwa na pointi tatu.
Leave a comment