May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taifa Stars kibaruani CHAN dhidi ya Zambia

Spread the love

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo kwa mara ya kwanza itashuka dimbani dhidi ya Zambia, katika michuano ya kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani inayofanyika Cameroon. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa kundi D, utachezwa majira ya saa 1 usiku kwenye Uwanja wa Omnisports uliopo kwenye mji wa Limbe, Cameroon

Hii itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kukutana kwenye michuano hiyo wakiwa kwenye kundi moja kama ilivyotokea mwaka 2009 ambapo Stars ilifuzu kwenye michuano hiyo ikiwa chini ya kocha Raia wa Brazil, Marcio Maximo.

Kuelekea kwenye mchezo huo huenda kocha wa Taifa Stars, Ettiene Ndayiragije akakosa huduma ya mshambuliaji wake John Bocco kutokana na kuwa na majeruhi ambayo aliyapata toka akiwa na klabu yake ya Simba licha ya kujumuishwa kwenye kikosi hiko.

Taifa Stars inahitaji ushindi kwenye mchezo huu wa leo ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu kwenye hatau ya robo fainali ya michuano hiyo.

Kwenye kundi hilo Stars yupo pamoja na timu za Mali, Zambia na Guinea.

error: Content is protected !!