TIMU ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ leo tarehe 2, Septemba inashuka dimbani katika Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kumenyana na timu ya taifa hilo kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 huko Quatar. Anaripoti Gabriel Mushi, Dar es Salaam … (endelea).
Mchezo huo utakaopigwa muda wa saa 10 jioni ni wa kwanza wa Kundi J ambalo linajumuisha timu za Madagascar, Benin, DR Congo na Tanzania.
Tarehe 7 Septemba, 2021 Taifa Star itamenyana na Madagscar kisha tarehe 10 Septemba itaifuata Benin kukamilisha mechi za mzunguko wa kwanza wa kundi lake.
Leave a comment