June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TAHLISO yashauri wapinzani kukubali matokeo

Spread the love

SHIRIKISHO la Vyuo vya Elimu ya Juu nchini (TAHLISO), limetaka vyama vya siasa vya upinzani kukubali matokeo na kuachana na propaganda za kuyapinga. Anaandika Hamisi Mguta …  (endelea).

Hayo yameelezwa leo na baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo katika mazungumzo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kuwepo kwa madai ya vyama pinzani kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Zainab Abdallah amesema hatua zinazoendelea kuchukuliwa na wagombea wa vyama mbalimbali kupinga matokeo hayo, zinachochea uvunjifu wa amani nchini.

Abdallah ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) amesema hali hiyo inachochea uvunjifu wa amani.

“Matokeo ya tume ni matokeo halali na hakuna kitakachobadilika kutokana na mashitaka katika mahakama ya kimataifa kwasababu nazo zina sheria zake na haitasimamia kesi baina ya chama na nchi isipokuwa inasimamia baina ya nchi na nchi,” amesema na kuongeza;

“Hata hivyo tunashukuru Chama Cha Mapinduzi na tunayo furaha kuweka historia ya kuwa na Makamu wa Rais mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza.”

Licha ya kusema matokeo hayo hayawezi kupingwa, ameomba wananchi kuachana na ukabira, udini na ukanda na badala yake kusimamia na kuhakikisha maendeleo yanakuwepo nchini.

error: Content is protected !!