MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imeeleza utabiri wake kwamba, kutakuwa na mvua kubwa kwa siku tano mfululizo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Kesho tarehe 23 Januari 2020, miko inayotabiriwa kunyesha mvua kubwa ni Lindi, Mtwara, Ruvuma na Morogoro Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA iliyotolewa leo tarehe 22 Januari 2020, imeeleza pamoja na kuwa na mvua hizo, kutakuwepo na upepo mkali pamoja na mawimbi makubwa katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba.
TMA imeeleza, mvua hizo na upepo unaweza kusababisha athari ikiwemo uharibifu wa miundombinu, makazi ya watu, shughuli za uvuvi, usafiri na kuanguka matawi ya miti.
Leave a comment