January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TAHA kuendeleza walimu wa mpira wa mikono nchini

Wachezaji wa mpira wa mikono

Spread the love

Chama cha mpira wa mikono nchini TAHA kinatarajia kuwa na kozi mbalimbali za walimu wa mchezo huo ili kuweza kukuza mchezo huo hapa nchini.

Katibu wa Chama cha Mpira wa Mikono Tanzania (TAHA), Nicholaus Mihayo aliuambia mtandao wa MwanaHALISi Online kuwa wameshaanza na hatua za awali ambapo kunakozi ambayo imemalizika wiki hii mkoani Tanga inayoshirikisha waalimu 17 wa shule za msingi na sekondari.

Mihayo amesema walimu wengi wanatakiwa kujitokeza ili kuweza kuchukua kozi hiyo na kuanza kutoa elimu kwa wanafunzi katika michezo ili kuweza kukuza mchezo huu hapa nchini.

 

error: Content is protected !!