Thursday , 23 March 2023
Home Kitengo Michezo TAFCA zaweka hadharani kamati tano
Michezo

TAFCA zaweka hadharani kamati tano

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA), limetangaza Kamati tano zitakazofanyakazi kama wizara za shirikisho hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza baada ya uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo uliofanyika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam juzi, Rais wa TAFCA, Adrian Nyangamale alisema pamoja na wizara hizo ameweka hadharani Jumuiya za shirikisho kwa malengo ya kutengeneza mifumo shirikishi kwa ajili ya kufanya kazi kama timu.

“Baada ya uchaguzi, tumeazimia kutangaza kamati tano na jumuiya mbili ambazo zitasaidia kuliendesha shirikisho, tunajipanga na kamati ya utendaji kuteua watendaji wa nafasi hizo Saba,” alisema Nyangamale.

Aidha Nyangamale alizitaja kamati hizo tano ni Mipango, Uchumi na Fedha huku kamati nyingine ni Haki, Sheria na Katiba nyingine ni Elimu na Mafunzo ya Ufundi ujuzi.

Kama