June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TaESA kulinda ajira za Watanzania nje

Afisa habari wa TaESA, Jamila Mbarouk

Spread the love

WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA), umeboresha utaratibu wa kuajiri Watanzania nje ya nchi ili kuepukana na kero zinazowakabiri wanapokwenda kufanya kazi huko. Anaandika Sarafina Lidwino….(endelea)

Kwa mujibu wa TaESA, Watanzania wengi hutoroshwa au kutoroka nchini kwa njia za panya, wakidhani haitafahamika lakini wakipatwa na matatizo huko ni lazima watarudishwa ili kufuata taratibu.

Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam leo, Afisa habari wa TaESA, Jamila Mbarouk, amesema lengo la kuweka taratibu hizo ni kulinda thamani na utu wa Mtanzania na kuweza kupata idadi kamili ya waajiriwa walioko nje ya nchi.

Amesema, kwa mwajiri yoyote anayetaka kumwajiri Mtanzania nje ya nchi ni lazma afuate taratibu za kuwepo na  mkataba wa ajira utakaokuwa umeridhiwa na Balozi wa Tanzania katika nchi husika, uwe umesainiwa na mwajiri na mwajiriwa ndani ya siku 14 kabla ya mwajiriwa kuondoka, kiwango cha mshahara na majukumu ya mwajiriwa.

Mbarouk ameongeza, “mkataba uonyeshe wajibu wa mwajiri endapo mwajiriwa atafariki au kuvunja masharti ya mkataba, uwe katika lugha ya Kiswahili na Kingereza, mwajiri atashughulikia vitu vyote vya muhimu kama Visa, tiketi na kibali cha ajira kutoka TaESA.

Amesema kuwa mwajiriwa huyo akishapata mkataba wake baada ya kuusoma na kutia saini atauwasilisha TaESA ili kuupitia na kuuridhia ukiwa umeambatanisha na barua ya mjumbe, mkataba wa kazi, barua ya mdhamini iliyosainiwa na mzazi au ndugu wa karibu, nakala ya kusafiria na Visa.

“Baada ya sisi kujiridhisha na taratibu zote kufuatwa ndipo mwajiriwa atapewa mafunzo elekezi kuhusu masharti yaliyopo ndani ya mkataba, mila, desturi, tamaduni na sheria za kazi kwenye nchi aendayo kufanya kazi,” amesema Mbarouk  

Amebainisha kwamba, baada ya kuwasili katika nchi husika, mwajiri anatakiwa ampeleke mwajiriwa kwenye ubalozi wa Tanzania ndani ya siku 7 tangu kuwasili, ili kuweza kujulikana kwa ubalozi kuwa muhusika ni raia wa Tanzania.

error: Content is protected !!