June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TADWU waituhumu serikali kumbeba bosi Tripple A

Spread the love

CHAMA cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU) kimeilaani serikali kwa kitendo cha kupuuza kesi ya dereva aliyeuliwa na muajiri wake kwa tuhuma za kupoteza mafuta yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda Zambia. Anaandika Aisha Amran … (endelea).

Akizungumza ofisini  kwake leo jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa chama hicho Shaaban Mdemu, amesema kuwa wanasikitishwa na serikali kutofuatilia  madai ya kesi inayomuhusu Mkurugenzi wa Tripple A, Hussein Jeta ambaye ndio anayetajwa kuhusika na mauaji kwa kumpiga risasi mbili mfanyakazi wake, David.

Amedai kuwa mshitakiwa ameachiwa huru na kuchukuliwa mtu mwingine ambaye hana hatia na pia si raia wa Tanzania ambapo kesi hii haijasikilizwa mpaka sasa.

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho, Abdallah Lubala amesema, naibu katibu wa chama hicho, Rashid Masanja  alifuatilia mwenendo wa kesi hiyo lakini hakuweza kufikia tamati hivyo kuibua madai ya  kuuliwa kwa kutiliwa sumu kwenye nyama aliyokula katika Hoteli ya River Side.

“Daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alithibitisa kuwa Masanja alikula nyama iliyotiliwa sumu na kupelekea kifo chake,” amesema Lubala.

Lubala amesema wanaiomba serikali kufuatilia mwenendo wa kesi ili wajue muuaji yuko wapi na tarehe ya kutajwa na kusikilizwa lini ili wafahamu  hatima ya mkurugenzi huyo wa Tripple A.

Aidha amesema wapo katika vikao vya kamati ambavyo inawashirikisa Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Ajira na Kazi, Chakua, vyama vya wamiliki wa malori na magari na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kujua hatima yao ya mikataba ya kazi, mishahara na posho.

error: Content is protected !!