Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Taasisi za sekta ya ujenzi Bara, Zanzibar zabadilishana uzoefu
Habari za Siasa

Taasisi za sekta ya ujenzi Bara, Zanzibar zabadilishana uzoefu

Spread the love

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, ameishauri Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na Wizara ya Ardhi, Maendeleo na Makazi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kuwekeza na kutoa fursa za kazi kwa vijana katika miradi ya ujenzi bara na visiwani ili kuwajengea uwezo wataalam wao wa ndani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amezungumza hayo leo tarehe 17 Novemba, 2022 kisiwani Unguja – Zanzibar, wakati akifunga mkutano wa tano wa mashauriano baina ya Wizara yake na Wizara hizo zinazoshabihiana katika majukumu ya taasisi zao.

Pia amesisitiza kudumisha ushrikiano baina yao ili kubadilishana uzoefu na kuongeza chachu katika mabadiliko chanya ya kiutendaji.

“Nchi yetu ina fursa nyingi, miradi mingi na hizi fursa tulizopata tuzitumie kwa kuwapa vijana kutoka bara na visiwani ili nchi yetu iweze kujenga watu katika usimamizi na ujenzi wa miundombinu bora na ya kisasa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa amesema kupitia Wizara yake inaendelea na mkakati wa kuwajengea uwezo wataalam wake kwa kuwashirikisha kwenye miradi mikubwa mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa viwanja vya ndege, barabara na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

“Wizara imepeleka wataalam mbalimbali katika miradi mikubwa ya ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Msalato, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), uboreshaji wa bandari, ujenzi wa meli na ujenzi wa barabara ya mzunguko (ring road) iliyopo Dodoma yote hii ikiwa ni kuwatengeneza vijana kuwa wabobezi katika kila eneo”, amefafanua Prof. Mbarawa.

Pia, amezishauri Wizara hizo ziweke mikakati ya kuongeza na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika kazi za ujenzi ambapo ushiriki wa kundi hilo bado hauridhishi.

“Nitoe wito kwa wenzetu wa SMZ kuweka juhudi katika kulisaidia kundi hili muhimu ili liweze kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa shughuli za ujenzi kwani lengo ni kukuza uchumi kuanzia ngazi ya familia kwasababu ukimkomboa mwanamke kiuchumi, unakuwa umeikomboa familia nzima”, amefafanua Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ametoa msisitizo kwa Wataalam wa Sekta ya Ujenzi kuhakikisha kazi zinafanyika kwa wakati na kwa ubora ili thamani ya fedha ipatikane na hatimaye watanzania waweze kujengewa miundombinu bora na ya kisasa.

Awali akifungua mkutano huo wa mashirikiano baina ya Wizara hizo, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukzui, Mhe. Masoud Ali Mohammed, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, amewataka wataalam hao kujifunza kutoka pande zote mbili za Muungano namna ambavyo wanatekeleza majukumu mbalimbali na hivyo kuyachukua yale mazuri kwa lengo la kuboresha katika utendaji kazi.

Katika mkutano huo Mawaziri hao wameshuhudia utiaji wa saini wa hati mbili za makubaliano, moja ikiwa baina ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (SMZ) na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi – SMT) kuhusu Bodi za usajili wa wataalam wa sekta ya ujenzi na ya pili ni baina ya Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) na Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROADS).

Mkutano wa tano wa mashirikano baina ya taasisi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (SMT) na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi pamoja na Wizara ya Ardhi, Maendeleo na Makazi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imefanya vikao kuanzia ngazi ya wataalam, ngazi ya Makatibu Wakuu na ngazi ya Mawaziri ambapo pamoja na mambo mengine watalaam walipata fursa ya kutemebelea na kubadilishana uzoefu katika baadhi ya miradi inayosimamiwa na Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROADS) na Wakala Majengo Zanziba (ZBA).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!