June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Taasisi yabeza awamu za JK na Mkapa

Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete

Spread the love

CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi stadi, Ushauri, Habari na Utafiti (RAAWU),  kimesema ni serikali ya awamu ya tano pekee ndiyo iliyokubali kufanyia kazi ushauri wao juu ya mambo mbalimbali kwa kipindi cha miongo miwili iliyopita, anaandika Christina Haule.

Chama hicho kilianzishwa mwaka 1994 na kimesema kwa miaka yote hiyo serikali imekuwa ikipuuzia zaidi ya mambo 40 waliyoyafikisha serikalini ili yafanyiwe kazi kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.

“Tulipendekeza maazimio 40 ambayo yangeleta maendeleo kwa wananchi kwa kuyapeleka serikalini lakini hakuna lililofanyika kwa kipindi chote cha nyuma, ni sasa hivi tu katika utawala wa Rais John Magufuli ndiyo tunaona yanafanyiwa kazi,” amesema Aldegunda Mgaya, Katibu Mkuu wa RAAWU.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 5 wa RAAWU uliofanyika mkoani hapa ulioenda sambamba na uchaguzi wa viongozi wapya wa chama hicho.

Baadhi ya mambo ambayo chama hicho kinadai kuwa kiliyapendekeza ni pamoja na athari za ubinafsishaji, ambapo kwa sasa Rais Magufuli anasisitiza Tanzania ya viwanda na akianza kuvifufua vile vilivyokuwa vimebinafsishwa na kutoendelezwa.

Suala la kodi na sera zake ambapo kwa sasa uongozi uliopo madarakani umeweka kipaumbele juu ya mambo hayo na kusimamia suala zima la makusanyo ya kodi ili kuliongezea pato Taifa.

Mgaya ametaja azimio lingine kuwa ni kilimo kubaki kuwa uti wa mgongo na kila mkoa uwe na zao moja kuu la chakula na biashara.

Kwa upande wake Nickolaus Mgaya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA), amewaasa wanachama hao kuzingatia demokrasia katika chaguzi zao ili kupata viongozi wenye nia thabiti ya kukiongoza chama hicho.

“Jitihada za kupata viongozi bora zitakisaidia chama chenu kutambulika na Serikali na hata mapendekezo yenu kupewa msukumo unaohitajika,” amesema.

error: Content is protected !!