March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Taasisi ya Tulia Ackson yatembeza bakuri kwa wadau

Tulia Ackson

Spread the love

TAASISI ya Utamaduni wa Ngoma za Asili ( Tulia Traditonal Dances) imewaomba wadau mbalimbali waliosaidia kufanikisha tamasha lao kufanya hivyo tena kwa mwaka 2018, anaandika Angela Willium.

Mmiliki wa taasisi ya Tulia Trust, Tulia Ackson amesema mashindano ya mwaka 2018 yatakuwa na washiriki wa mikoa 31 ya Tanzania hivyo tamasha litakuwa kubwa na lengo ni kukuza utalii wa nchi kwani mashindano haya yanahudhuriwa na watu wa nchi tofauti.

“Mashindano ya ngoma za asili mwaka huu yalishirikisha mikoa 17, mwakani tunatarajia kuwa na vikundi vya ngoma kwa mikoa yote ya hapa Tanzania hivyo tunahitaji wadau wa kutosha ili mashindano yaende vizuri kama mwaka huu,’’ amesema Tulia.

Amesema lengo la kuwepo kwa mashindano hayo kukuza maendeleo ya uchumi hapa nchini kwa wageni watakapokuja watafurahi kuona utamaduni wa ngoma za asili.

Aidha, mwakilishi wa Naibu Waziri wa Michezo, Sanaa na Habari, Liliy Bayeko amesema Tulia Trust iendelee kufanya mashindano hadi itakapofika kimataifa.

Mashindano ya ngoma za asili Tulia Trust yalianzisha mwaka 2016 kwa mikoa sita ambayo yalishirikisha vikundi vya ngoma.

error: Content is protected !!