January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taasisi ya Mwl Nyerere Kuunguruma kesho

Spread the love

TAASISI ya Mwalimu Nyerere ambayo malengo yake makuu ni kulinda na kudumisha amani, umoja na maendeleo ya watu wote nchini, itaunguruma kesho katika mdahalo ambao imeuwandaa. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Mdahalo huo unalenga kusisitiza umuhimu wa kulinda tunu kuu za taifa za: amani umoja na haki.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Joseph Butiku kwa MwanaHALISI Online inasema “ Taasisi ya Mwl Nyerere imeandaa mdahalo ili kusisitiza na kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa kuzingatia, kulinda na kutetea tunu za taifa letu.”

“Mdahalo utashirikisha wadau wote wa uchaguzi wakiwemo vyama vya siasa, taasisi za kitaaluma, vyombo vya habari, vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu, vyama vya wafanyakazi, wazee na wastaafu, vijana, wanawake na makundi mengine ya kijamii,” inasema taarifa hiyo.

Aidha, mdahalo huo utafanyika ukumbi wa mikutano hoteli ya Blue Pearl, Ubungo jijini Dar es Salaam saa 8 mchana hadi saa 12 jioni ukihutubiwa na Joseph Butiku, Getrude Mongela na Prof. Paramagamba Kabudi.

error: Content is protected !!