May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taasisi ya Mwalimu Nyerere, wadau kujadili demokrasia

Julius Nyerere, Hayati Baba wa Taifa

Spread the love

 

TAASISI ya Mwalimu Nyerere inatarajia kukutana kesho tarehe 17 Januari jijini Dodoma kwa lengo la kufanya majumuisho ya maoni iliyokuwa ikiyakusanya kwa wadau kwa lengo kuwafanya watanzania kuwa na roho ya uzalendo. Anaripoti Danson Kaijage,Dodoma …  (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka taasisi hiyo ambayo imetolewa leo tarehe 16 Januari, 2022 na Aisa Mushi, Afisa mipango wa Mradi kufanya majumuisho ambayo yatakuwa na malengo wa kuifanya Tanzania kuwa salama.

Majumuisho hayo yanatokana na makongamano mbalimbali ambayo yalikuwa yakifanyika kwa kuwashirikisha wadau kwa lengo la kulifanya taifa kuwa katika mwelekeo mmoja.

Kutokana na hali hiyo Taasisi ya Mwalimu Nyere imewaalika watu mbalimbali kwa lengo la kutoa ushauri na mapendekezo na zaidi ni katika kusimamia demokrasia.

Amesema Tanzania ni nchi ya amani na watu wake wanatakiwa kuwa na amani sambamba na kuwa na uhuru wa kujieleza.

“Watanzania wanatakiwa kuwa huru na kupata haki ya kujieleza sambamba na kueleza mahitaji yao kwa kuzingatia misingi bora ya ya sheria za nchi.

“Yapo naneno mengi hasa ya kudai katiba mpya na tume ya uchaguzi haya mambo yanatakiwa kujadiliwa kwa kina na kutoa hoja za nguvu.

“Nawashangaa watu ambao wanasema kuwa wanaonewa je, wanaonewa na nani, nani anawatia uwoga! je wanajieleza kwa kufuata utaratibu?

“Haya mambo yote tutayajadili kesho na kuweka mapendelezo nini kifanyike hata kama tukipata Katiba mpya lakini kama hakuna demokrasia ya kweli hiyo katiba hiyo itakuwa ni bure” amesema.

error: Content is protected !!