September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taasisi ya Mo Dewji, Timu ya Simba watoa msaada Muhimbili

Spread the love

TAASISI ya Mohammed Dewji (Mo Dewji Foundation) na Timu ya Mpira wa Miguu ya Simba (SSC) wamekabidhi vituo vya kuosha mikono, sabuni pamoja na vitakasa mikono katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Pia, msaada huo uliokabidhiwa leo Alhamisi tarehe 21 Mei, 2020, unatolewa kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) lengo ikiwa ni kusaidia kudhibiti maambukizi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (Covid 19).

Akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez amesema ujenzi wa vituo hivyo ni mwanzo wa zoezi ambalo litaendelea hivi karibuni katika hospitali nyingine kama Mloganzila, Mwananyamala, Temeke na Amana zote za jijini Dar es Salaam.

“Tunatumia nafasi hii kuwashukuru uongozi wa hospitali zote tatu na kila mmoja wenu ambaye alishiriki kufanikisha kazi hii pamoja na kuwepo kwa changamoto ugonjwa wa Codiv19, ” amesema Barbara.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Timu ya Simba, Senzo Mazingiza amesema wanatambua mchango mkubwa unaofanywa na watumishi wa sekta nzima ya afya, hivyo wameona wachangie sabuni pamoja na vitakasa mikono.

Wakipokea msaada huo, Mkurugenzi wa Tiba, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Hedwiga Swai, Mkurugenzi wa Tiba wa MOI, Dk. Samuel Swai na Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya ya Moyo wa JKCI, Dk. Tulizo Shemu wameshukuru msaada huo kwa kuwa utasaidia kupunguza kazi ya usimamizi wa kuosha mikono ambayo mwanzo ilibidi ifanyike na walinzi katika milango mikuu na milango ya kuingia majengo yote ya hospitali.

error: Content is protected !!