January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taasisi ya Kiislam yafikia lengo uchangiaji damu

Spread the love

JUMUIYA ya Alhalaki Islam (JAI) imefanikisha zoezi la uchangiaji damu leo kwenye Hospitali ya Wilaya ya Temeke na Mbagala Zakiem Jijini Dar es Salaam ambapo zaidi ya lita 130 zimepatikana, Anaandika Faki sosi … (endelea).

Kiongozi mkuu wa Jumuiya hiyo Shekh Yahya Masao amesema kuwa, zoezi hilo ni endelevu na kwamba litakuwa linafanyika kila baada ya miezi minne.

Pamoja na uchangiaji damu huo, taasisi hiyo hutoa msaada kwa wagonjwa wasiokuwa na ndugu kwenye hospital 32 za umma nchi mzima.

“Huduma ambazo tunazitoa kwa wagonjwa wasiomudu au wasiokuwa na ndugu ni pamoja na kuwanunulia dawa, maji, kuwapikia chakula na kuwaosha endepo mgonjwa atakuwa hajiwezi.

“Kwa hapa Dar es Salaam misaada hiyo tunatoa kwenye hospital tano ambazo ni Taasisi ya Saratani (Ocean Road), Hospital ya Taifa ya Muhimbili, Mwananyamala, Temeke na Vijibweni,” amesema Shekh Masao.

Amesema kuwa, damu hiyo itahifadhiwa kwa ajili ya dharura itakayotokea ikiwa ni pamoja na ajali, wajawazito wakati wa kujifungu.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Dk. Amani Malima ambaye alijitokeza na kutoa damu kwenye zoezi hilo ameipongeza taasisi hiyo ya Kiislamu na kuwataka jamii na tasisi nyengine zijiweke utaratibu wa kuchangia damu mara kwa mara kutokana na mahitaji yake. Amesema kwamba hospitali hiyo inahitaji chupa 40 za damu kila siku.

Dk. Amani amesema kuwa, taasisi hiyo imechangia kupatika kwa zaidi ya lita 150 na kuwa damu hiyo itasaidia kuokoa uhai wa zaidi ya watu 100.

Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallaha Chaulembo ambaye ni miongoni mwa waliotoa damu amesema kuwa, taasisi hiyo ni ya kuigwa hapa nchini kutokana na mchango walioutoa.

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea akiwa miongoni mwa wachangiaji amesema makundi mengine ndani ya jamii yanapaswa kuiga mwenendo wa taasisis hiyo kwani kuchangia damu ni moja ya kanuni za afya pele damu inapokuwa nyingi.

“Ofisi yangu imehamasisha vijana wa jogging kujitolea damu ambapo wengi wao wameitikia wito huo,” amesema Mtolea.

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Tawi la Temeke, Khareed Mzezere amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu.

Anasema wamekuwa wakihudumia wagonjwa kwenye Hospitali ya Temeke kwa kushirikia na wauguzi kwenye hospitali hiyo.

Naibu Meya wa Halmashauri ya Temeke, Faisal Salumu ambaye ni miongoni mwa wachangiaji damu amesema kuwa, damu haiwezekani kupatikana kwa mchango wa fedha na kuwa ni lazima watu wachangie damu ili kuwa msaada kwa mgonjwa wa dharura.

“Mbadala wa damu sio kununua, ni lazima tuichangie ili itusaidie wenyewe kwani sisi ndio wagonjwa watarajiwa licha ya kukithiri kwa ajali na dharura za kujifungu akina mama. Kwa hiyo damu inahitajika zaidi kwenye afya ya mwanaadamu,” amesema Faisal.

Shaabani Shekigenda amabye ni mlemavu wa macho amejitokeza kwenye uchangiaji huo. Anasema kuwa ana uwezo wa kuchangia lita sita kwa siku kutokana na ulaji wake wa matunda.

Hata hivyo amesema kwamba amechangia damu mara 22 na amedumu kwenye uchangiaji wa damu kwa miaka mitano sasa.

Zidi ya watu 130 wamejitokeza kwenye uchangaji huo wa damu ambapo wiki iliyopita jumuiya hiyo ilijitokeza na kufanya zoezi hilo kwenye Hospital ya Amana na Hospita ya Taifa ya Muhimbili ambapo watu zaidi ya 100 walijoitokeza. Zoezi hilo linaendeleakesho kwenye Hospital za Mwananyamala, Vijibweni, Tanga, Kibaha na Kilimanjaro kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa sita.

Zoezi hili litafanyika kitaifa siku ya tarehe 23 mwezi huu ambapo itaendana na Siku ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammadi (S.A.W).

error: Content is protected !!