June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taasisi ya Elimu Watu Wazima ‘yatumbuliwa’

Spread the love

PROFESA Eustelia Bhalalusesa, Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufunzi amemuagiza Dk. Tidelice Mafumiko, Mkurugenzi Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuwavua madaraka wakufunzi wa kazi watatu, anaandika Happyness Lidwino.

Wakufunzi hao wanaotakiwa kuvuliwa madaraka ni Wotuga Muganda wa Dar es Salaam, Senorina Kateule wa Dodoma na Steward Ndandu wa Mwanza na Geita.

Akizungumza wa waandishi leo Jijini Dar es Salaam Prof. Bhalalusesa amesema, watu hao wanatakiwa kuvuliwa madaraka kwa kukiuka utaratibu wa kazi na kufanya udanganyifu kwa wanafunzi.

Amesema, watumishi hao wenye dhamana ya kusimamia elimu ya watu wazima katika mikoa hiyo walifanya udanganyifu kwa kuwachukuwa wanafunzi wasiokidhi vigenzo vya ufaulu wa alama 100-250 (kiwango cha ufaulu wa shule za serikali) na kuwapangia Shule za Serikali licha ya kuwa na alama ndogo.

“Tumepokea malalamiko mengi kutoka kwa wazazi na wanafunzi wakidai kuwa, watumishi hao waliwaandikia barua za kujiunga na shule za serikali na walipofika katika shule hizo, hawakupokelewa kutokana na alama zao kutokidhi vigezo. Hivyo kitendo hicho ni cha upotoshaji,” amesema.

Hivyo, utaratibu uliotumika kwa mikoa hiyo wa kuchagua wanafunzi kujiunga katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kupitia halmashauri na mikoa utaratibu haukua sahihi kufuata upotoshwaji wa makusudi wa kuwachagua wanafunzi chaguo la pili japo hawana vigezo.

Hatua hiyo imesababisha mkanganyiko mkubwa kwa wazazi na walezi ambao wamekuwa wakiamini watoto wao wamefaulu na wamechaguliwa kujiunga na shule za serikali hivyo kuwa na matumaini ya kuhusika na utaratibu wa sasa wa elimu bure.

Prof. Bhalalusesa ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto wanaosoma katika vituo vya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika katika mikoa mingine ambao wamechaguliwa kwa utaratibu unaolalamikiwa watoa taarifa haraka katika Wizara husika ili hatua stahiki zichukuliwe.

error: Content is protected !!