July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuelekea Sikukuu ya Pasaka

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova

Spread the love
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

PRESS RELEASE

02/04/2015TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TAHADHARI YA KIUSALAMA KUELEKEA SIKUKUU YA PASAKA 2015.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeweka mikakati ya mpango kazi kama ifuatavyo:-

• Limepanga kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi cha Zimamoto na uokoaji, Kampuni binafsi za ulinzi, Vikosi vya uokoaji wakati wa majanga, na vikundi vya Ulinzi Shirikishi ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo zinazoweza kujitokeza.

• Tumejipanga kwa ulinzi wa hali ya juu kwa kutumia askari wetu wa doria za miguu, doria za magari, kikosi cha mbwa na Farasi, kikosi cha wanamaji, Usalama barabarani, askari wa upelelezi, Helkopta ya Polisi, n.k.

• Zitakuwepo doria za Magari, doria za pikipiki na doria za miguu katika barabara zote muhimu.

• Wananchi wanashauriwa kusherehekea siku ya Pasaka katika ngazi ya familia au kukusanyika katika mitaa kwa amani wakisherehekea pamoja na majirani, marafiki n.k.

• Kutokana na sababu za kiusalama na matishio mbalimbali katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, Jeshi limejipanga kushughulikia viashiria vya matukio ya Kigaidi au ujambazi wa kutumia silaha kubwa.

Nimepiga marufuku disko toto kufanyika katika kumbi mbalimbali jijini Dar es Salaam kutokana na kumbi hizo kutokidhi viwango vya kiusalama, hivyo kukosa sifa.

• Wananchi wanapoona dalili zozote au maandalizi ya uvunjifu wa amani watoe taarifa mapema iwezekanavyo katika vituo vya Polisi vya karibu au wapige simu namba 111 na 112 ili hatua zichukuliwe kwa haraka.

• Madereva wanatakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi, wasiwe walevi, magari au pikipiki zenye sauti kali/zenye kuleta mshtuko nazo nimarufuku.

• Aidha, Kikosi cha Polisi Wanamaji (Marine Police) kitafanya doria kwenye fukwe za Bahari na maeneo yote ya Bahari jijini Dar es Salaam. Patakuwepo Helkopta ya Jeshi la Polisi ikifanya doria kuzunguka jiji la Dar es Salaam na askari wa Kikosi cha Mbwana Farasi nao watahusika na doria.

• Polisi watatoa ulinzi katika fukwe za bahari, kwa kuweka vituo vya Polisi vya muda vinavyohamishika (Mobile Police Station) ili kutoa msaada wa haraka pindi unapohitajika. Pia askari wa kutosha watakuwepo kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani.

• Aidha, kwa urahisi wa mawasiliano wananchi wasisite kutoa taarifa za uhalifu kwa namba muhimu za simu zifuatazo:
1. RPC ILALA: Mary Nzuki – DCP 0715 009 980
2. RPC TEMEKE: Kihenya Kihenya –ACP 0715 009 979
3. RPC K’NDONI Camillius Wambura – ACP 0715 009 976

S. H. KOVA,

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.

 

error: Content is protected !!