January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TAA wawakomalia wahasibu

Spread the love

CHAMA cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimetishia kuwaondoa wahasibu waliokuwepo kwenye daftari la chama hiko endapo watakiuka taratibu na maadili ya kazi kulingana na matakwa ya chama hicho ikiwemo ya rushwa, wizi na ufisadi. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho, Fred Msemwa katika mazungumzo yake na wanahabari wakati akitoa pongezi na kuunga mkono kwa jitihada za serikali ya awamu ya nne juu ya ukusanyaji wa mapato.

Msemwa amesema kuwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu, wanatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa taaluma zao kwa kufuata miongozo ya sheria Na.33 ya 1973 inayosimamia taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu Tanzania.

Amesema kuwa chama hicho hakitasita kumundoa mhasibu yoyote atakayeshiriki katika wizi na mambo mengine kinyume na matarajio ya wananchi ataondolewa haraka.

“Hatuna idadi kamili ya waliokiuka taratibu za chama lakini tumepata taarifa kuwa wapo wanaokiuka taratibu hizo,” amesema Msemwa.

error: Content is protected !!