July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Szubin: Rais Putini mla rushwa

Spread the love

RAIS wa Urusi, Vladmir Putini anatajwa kuwa miongoni mwa wala rushwa, kashfa hiyo inatolewa ikiwa ni siku chache baada ya rais huyo kuhusishwa na kifo cha jasusi wa zamani wa nchi hiyo Alexander Litvinesko.

Kauli ya Rais Putini kuhusishwa na rushwa imetolea na Wizara ya Fedha ya Marekani, Adam Szubin ambaye alieleza kwenye Kituo cha Utangazaji cha Uingereza (BBC) wakati wa Kipindi cha Palorama.

Uhusiano wa kauli hiyo unaelezwa ni kutokana na hatua ambazo tayari maofisa wa Serikali ya Marekani wamechukua kwa kukwawekea vikwazo wasaidizi wa Putin.

Szubin anayesimamia vikwazo vya Wizara ya fedha vya Marekani ameeleza kuwa Putin ni mla rushwa wa siku nyingi na kwamba Serikali ya Marekani inatambua suala hilo kwa muda mrefu.

Szubin ameeleza kuwa Putin amekuwa akifanya upendeleo kutokana na kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa yake na watu wanaomzunguka huku akikandamiza wengine.

“Tumemwona akiwaneemesha marafiki zake na watu wake wa karibu na kuwakandamiza wale ambao sio marafiki wake kwa kutumia rasilimali za taifa kama utajiri wa nishati au mikataba baina yao na serikali amekuwa akitoa maagizo iwanufaishe wale ambao anaamini watamnufaisha na kuwatenga wale wasiomnufaisha. Kwangu mimi hiyo hiyo ni sura ya rushwa,” amenukuliwa Szubin.

Si mara ya kwanza Putin kuhusishwa na kashfa ya rushwa ambapo mwaka 2007 kwenye ripoti ya siri ya Shirika la kijasusi la CIA, lilieleza kuwa rais huyo wa Urus ana utajiri wa Dola za Marekani zinazofikia 40 bilion ambapo baadaye Putin alieleza kuwa ni propaganda tupu.

error: Content is protected !!