January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Syria mpya yaanza kuonekana

Spread the love

MAUAJI, mateso ndani ya nchi ya Syria huenda yakakoma baada ya makundi ya waasi nchini humo kuridhia kusimamisha mapigano na kuingia kwenye mazungumzo mwezi ujao.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa mkutano wa siku mbili mfululizo nchi Saud Arabia ambapo makundi hayo ya waasi yalikutana kwa ajili ya mazungumzo ya awali.

Waasi hao kwa tamko moja wamekubaliana kuweka silaha chini na kutoa nafasi kwa majadiliano kuanza huku sharti la kumtaka Rais wa Syria, Bashar Al Assad kuachia ngazi kabla ya majadiliano hayo kuanza wakilifuta.

Awali makundi hayo yalitoa shatri kwamba, ili kuweka silaha chini na kuingia kwenye mjadala ni lazima Rais Al Assad ang’oke madarakani jambo ambalo rais huyo alilipinga na kueleza haliwezekani.

Mkutano huo nchini Saudi Arabia uliongozwa na mwenyekiti wake Abdulaziz Al-Sager ameeleza hatua gani itafuata baada ya mazungumzo hayo.

Ameeleza kuwepo kwa mkutano ambao utaamuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) Januari na kwamba utakua ni mkutano baina ya upinzani na serikali ya Syria ambapo utachukua siku 10 za mwanzoni mwa Januari.

Pamoja na hivyo, wapinzani wameeleza kuwa Assad ataachia madaraka baada ya kutengeneza serikali mpya huku Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje nchini Marekani, John Kirbly akipongeza hatua hiyo.

error: Content is protected !!