May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sven atoa sababu kuikacha Simba

Sven Vandenbroeck

Spread the love

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema, ameondoka ndani ya timu hiyo ili kumwezesha kuwa na uwiano kati yake na kazi, familia na maendeleo binafsi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Sven ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 8 Julai 2021 kupitia akanuti yake ya Instagram ikiwa ni siku moja imepita yangu Bodi ya Simba kutoa taarifa ya kuanachana na kocha huyo.

Simba iliachana na Sven ikiwa ni siku moja kupita, tangu alipofanikiwa kuivusha hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuitoa FC Platinum ya Zimbabwe kwa uwiano wa magoli 4-1.

Sven ameweka picha akiwa pamoja na wachezaji na benchi la ufundi wakishangilia ushindi wa 4-0 walioupata kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya FC Platinum. Katika mchezo wa kwanza dhidi ya timu hiyo uliochezwa Harare, Zimbabwe, Simba ilifungwa 1-0.

Amesema, ameamua kuchukua uamuazi huo ili kutafuta mizania sawa kati yake na kazi, familia na maendeleo yake binafsi.

Sven amewashukuru wachezaji na mashabiki kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote akiwa klabuni hapo.

Raia huyo wa Ubelgiji ambaye tayari amekwisha kuondoka nchini Tanzania, amemshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed Dewji na Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez jinsi walivyomsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake.

Sven amesema, Mo na Barbara walijaribu kumshawishi hadi hatua ya mwisho kubaki kukifundisha kikosi hicho lakini ilishindikana.

Sven aliyejiunga na Simba mwaka 2019, ameondoka akiwa ameichia mafanikio msimu uliopita kwa kutetea kombe la ligi kuu, kutwaa kombe la shirikisho na ngao ya jamii na kuifukisha hatua ya makundi.

Simba imepangwa kundi A pamoja na timu za Al Merrikh (Sudan), AS Vital (DRC Congo) na Al Ahly ya Misri.

error: Content is protected !!