Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Susan Lymo: Napigania Jimbo la Kinondoni 2020
Habari za Siasa

Susan Lymo: Napigania Jimbo la Kinondoni 2020

Suzan Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum Chadema
Spread the love

SUSAN Lymo, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ni miongoni mwa wanasiasa wanaonyatia Jimbo la Kinondoni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na MwanaHALISI Online, Lymo amesema, hii itakuwa mara ya pili kujitokeza na na kupigania ubunge kwenye jimbo hilo.

Nimeamua “Sio mara ya kwanza, hii ni mara ya pili. Mwaka 2015 nilitia nia na nilienda kwenye kura za maoani ndani ya chama. Kura zilipopigwa, nilishika nafasi ya pili.

“…lakini jimbo likaenda Ukawa (uamuzi wa muungano usio rasmi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi), vinginevyo Kamati Kuu (ya Chadema) ingeweza kumteua huyo wa kwanza ama wa pili kwa sababu tulipishana kwa kura nne tu,” amesema Lymo.

Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, jimbo hilo alishinda Maulidi Mtulia wakati huo akiwa Chama cha Wananchi (CUF), ni jimbo ambalo Ukawa ulioundwa na Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD uliamua kuliacha jimbo hilo kwa CUF.

Hata hivyo, Desemba 2017, Mtulia alihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), jambo lililosababisha uchaguzi kwenye jimbo hilo kurudiwa. CCM ilimteua Mtulia kuwawakilisha kwenye uchaguzi huo, alishinda.

Susan Lyimo, Aliyekuwa Mbunge Viti Maalum (Chadema Kinondoni)

Amesema, sababu kubwa iliyomsukuma kurejea kujipima ubavu tena, ni dhamira yake ya kuwa na uwanda mpana wa kuwatumikia wananchi tofauti na nafasi ya ubunge wa Viti Maalum.

Amefafanua kwamba, Mbunge wa Viti Maalum anakuwa na uwanda mfupi wa kuwatumikia wananchi na kwamba, kuna baadhi ya maeneo ambayo hata kama ana uwezo nayo, hawezi kuingia ama ‘kupush’ ili jambo fulani lifanikiwe

“Ninagombea kwa sababu mimi ni Mbunge wa Viti Maalum wa Kinondoni, wakati nateuliwa kulikuwa na majimbo manne yaani Ubungo, Kawe, Kibamba na K’ndoni yenyewe, mimi nilikuwa mlezi wa majimbo hayo.

“Unapokuwa mbunge unakuwa diwani, hivyo ninajua changamoto nyingi za kata hizi 10 za Kinondoni ambazo nimezitembelea zote,” amesema Lymo na kuongeza:

“Unapokuwa mbunge wa jimbo, ni tofauti na viti maalum, kwanza; kunaingia kwenye Kamati ya Fedha na Mipango, maana fedha nyingi takribani asilimia 70 zinakwenda halmashauri zetu na huko ndio tunaibua miradi.”

Pili; amesema, Jimbo la Kinondoni bado lina changamoto ya miundombinu sambamba na vituo vya afya kwa mujibu wa sera ya nchi.

Hivyo, anagombea ili kupata uwanda mpana kuhakikisha anasimamia utatuzi wa kero hivyo, na kwamba ubunge wa jimbo unampa nafasi ya kusimamia na hata kuhoji kwa ajili ya wananchi wake.

“Sera inasema kila Kata iwe na kituo cha afya, hili halipo na kusabaisha misongamono kwenye vituo vichache vilivyoo. Ukiwa Mbunge wa Vitu Maalum unakuwa na uwanda mchache, unaona kuna kuwa na vikazo ya kufuatilia baadhi ya mambo. Hivyo unahitaji jimbo ili ukifanya kazi inaonekana,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!