August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sumu yazua taharuki Democratic

Spread the love

POLISI jijini New York nchini Marekani wamekanusha taarifa za sumu iliyopatikana kwenye ofisi ya Mgombea Urais wa chama cha Democratic Bi. Hillary Clinton huko Manhattan, anaandikaWolfram Mwalongo.

Sintofahamu imegubika taifa hilo kufuatia kusambaa kwa tarifa za kupatikana kwa bahasha yenye poda nyeupe iliyodhaniwa kuwa na sumu kwenye ofisi ya Mgombea huyo anayetishia kuibwaga Republican katika uchaguzi mkuu wa Novemba mwaka huu.

Polisi wamedai uchunguzi wa awali unaonesha poda hiyo ilitumika kufanya matengenezo ya jengo hilo hivyo kuwataka wananchi na wanachama wa Republican kupuuza taarifa hizo.

Wakati shughuli za uchaguzi zikiendelea kupamba moto nchini humo tukio hilo linakuwa la pili ambapo tarehe 17 mwezi huu chupa iliyokuwa na kimiminika kilicho sababisha mlipuko kwenye Ofisi ya Republican katika Jimbo la Carolina kaskazini. Huku Mgombe wa Chama hicho Donald Trump akidai kuwa tukio hilo lilikuwa ni shambulio la kigaidi kwakuwa chama chake kinaelekea kushinda, ingawa ameshindwa kusema wazi endapo atashindwa atakubali matokeo au laa!.

Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya kisia ndani na nje ya taifa hilo wamedai kuchomwa kwa ofisi za Republican kunatoka  na chuki ya sera za kibaguzi za Trump hasa ukanda huo unaoongoza kwa kuwa na wamarekani weusi wanaoonyesha wazi hawana mpango na mgombea huyo.

 

error: Content is protected !!