August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sumaye – sasa tunaelekea vijijini

Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, Fredrick Sumaye, amesema chama chake kitazunguka nchi nzima kuelimisha wananchi juu ya haki zao, anaandika Catherine Kayombo.

Amesema elimu hiyo itatolewa katika vijiji na vitongoji vyote nchini, ili wananchi waweze kujua haki zao, ili kuweza kuamka na kupinga demokrasia kandamizi inayoota mizizi.

Hakutaja tarehe ya kuanza mpango huo, lakini alisema kuwa hadi mwisho wa mwaka kesho nchi nzima itakuwa imeelimishwa kuhusu haki za raia.

Sumaye amesema hayo leo katika ofisi za kanda, Magomeni, Dar es Salaam, alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusu kile alichoita “mambo yanatotuhusu sote kwa maslahi ya taifa.”

Alizungumzia nafasi ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa, mfumo wa demokrasia kandamizi, utawala wa demokrasia sahihi ya vyama vingi, utawala bora na demokrasia kandamizi, na kazi ya vyama vya upinzani.

“Watu wanadhani udikteta ni lazima uingie madarakani kwa mabavu. Hapana! Unaweza kuwa dikteta hata kama umeningia madarakani kwa kura, mradi mfumo uliotumia ni demokrasia pingamizi,” alisema.

Moja ya haki za msingi ambayo Sumaye alizungumzia ni haki ya kutoa na kupata habari, ambayo pia inalindwa na ibara ya 18 ya katiba ya nchi.

error: Content is protected !!