Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sumaye, MO watibua hali ya hewa bungeni
Habari za Siasa

Sumaye, MO watibua hali ya hewa bungeni

Spread the love

SAKATA la kubadilishwa hati ya mashamba ya  makubwa ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye na Mfanyabiashara, Mohamed Dewji ‘MO’ limeibuka bungeni wakati wabunge wakichangia katika taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hali hiyo iliibuliwa Bungeni na Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa (Chadema) alipokuwa akichangia huku Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) kuibuka kuwa kinachosumbua ni mashamba ya Sumaye ambayo hajaendelezwa.

Katika mchango huo Mch. Msigwa alisema kuwa licha ya kuwa haoni shida ya unyang’anywaji wa mashamba lakini taratibu zinazofanyika siyo sahihi.

Mch. Msigwa alisema kuwa pamoja na mambo mengine kamati haikuweza kuweka baadhi ya mapendekezo ya kamati kutokana na kutoyaweka katika mapendekezo hayo ambayo ni kuitaka serikali kuunda kamati ya kuchunguza jinsi ya unyang’anywaji wa mashamba hayo.

“Lakini kuna kitu ambacho nataka kusema wakati tupo kwenye kamati kuna taarifa ambayo ilitakiwa iingizwe lakini haikuweza kuingizwa ndani ya taarifa hii.

“Pamoja na sifa nyingi za mheshimiwa Lukuvi ambazo na mimi nilishawahi kumpa lakini suala hili la mashamba makubwa lina harufu mbaya ya rushwa na ukakasi,” alisema Mch. Msigwa.

Akichangia katika sekta ya Utalii, Mch. Msigwa alisema kuwa watalii waliosafiri duniani kote walikuwa zaidi ya bilioni nane na sekta hiyo ilitoa ajira zaidi ya milioni 275 duniani kote hiyo ilikuwa zaidi ya asilimia 11 ya ajira duniani.

“Na hiyo inaonesha kuwa sekta hiyo ilivyo na nguvu na inaajiri watu wengi na inazalisha shughuli mbalimbali nakumbuka waati huo serikali ilijaribu kupanua wigo kwa miaka kumi iliyopita serikali ilikuwa na uwezo wa kupokea watalii laki nane.

“Lakini mpaka leo pamoja na fursa nziri tulizonazo hatujaweza kufikisha watalii 1500 na hii inatokana na kutokuwa na mipango mizuri ya kuboresha sekta ya utalii,” alisema Mch. Msigwa.

Alisema serikali inahangaika kwa sababu hakuna mipango endelevu na kwa sababu hatufikilii kama taifa, katika wizara hii waziri aliyekaa muda mrefu ni Zakia Meghji na alikaa kwa sababu alikuwa akiwasikiliza wataalam.

Alisema kuwa nchi ya Tanzania ni kati ya nchi yenye vivutio vingi tungeweza kuwavutia watalii kwa sababu tunanyang’anyana na nchi nyingine.

“Lakini kwa bahati mbaya wizara hii imekuwa ikibadilishwa na mawaziri ambao wanaenda wanakuwa kama wajuaji tuna fukwe nyingi katika nchi yetu haizifuati.

“Na kama ikikuzwa sekta hiyo itaweza kuajiri watu zaidi ya laki nane kutokana na hali hiyo wizara inatakiwa kujitafakari ni jinsi gani ya kuweza kuweka utaratibu wa kuwaweza kuwakarimu wageni ambao ni watalii.

Akizingatia masuala ya usafi alisema kuwa utalii unakuwa wa ovyo ni pamoja na uchafu, kukosekana kwa miundombinu sambamba na kutokuwa na ukarimu wa kutosha kwa wageni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!