January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sumaye: Lowassa anastahili urais

Spread the love

WAZIRI Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ametangaza rasmi kuwa Edward Lowassa ni mgombea makini asiye doa, na anastahili kuchaguliwa ili aongoze taifa linalohitaji mabadiliko. Anaandika Jabir Idrissa … (endelea).

Amesema kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama kilichojifunika vyama viwili. Hakueleza kwa ufasaha tungo hiyo, labda akimaanisha chama hicho kinatumia mgongo wa dola kushikilia madaraka licha ya kukataliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu.

Akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya Lowassa anayegombea urais kupitia Chadema, kwa mamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) leo hii kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, Sumaye alisema anamuunga mkono Lowassa.

“Niko pamoja na Mhe Lowassa. Niko pamoja na Ukawa… pamoja nanyi wana mabadiliko. Siku ikifika ya Oktoba 25, pigeni kura zenu kwa mhe Lowassa na tutashinda tu,” amesema.

Amemtetea Lowassa kuwa amekuwa akizushiwa kashfa zisizo zake wakati inajulikana hata ndani ya CCM kuwa alichukua uamuzi wa kiuwajibikaji ili kumhifadhi mkubwa wake.

Mkubwa wa Lowassa ni Rais Jakaya Kikwete ambaye alimtosa Lowassa alipolazimu kujiuzulu uwaziri mkuu Februari 2008, kutokana na shinikizo la Bunge lilipojadili ripoti ya uchunguzi wa mazingira ya mkataba wa kufua umeme uliopewa Richmond Development Company (RDC).

Lowassa ambaye ndiye waziri mkuu wa kwanza wa Rais Kikwete baada ya kuingia madarakani Novemba 2005, katika hotuba yake fupi bungeni alisema hakufanya kosa lolote lakini kwa kuona kuwa tatizo lililosumbua wabunge wengi ni yeye kuwa waziri mkuu, “nimemuandikia Rais kumuomba nijuzulu.”

Sumaye amesema kama Lowassa ni dhaifu basi aliyemteua kuwa waziri mkuu wakati ule, ndiye aliyekuwa dhaifu hasa. Lakini alisema Lowassa si dhaifu na ana kichwa chenye uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi.

Ametaja mlolongo wa kashfa zilizoibuka wakati wa uongozi wa Rais Kikwete, akisema hakuna hata moja ilimhusu Lowassa.

Baadhi ya kashfa hizo ni EPA (2005), Escrow (2014) kama mfano lakini akasema Lowassa alichokifanya wakati wa kashfa ya Richmond, ni kuihifadhi serikali.

Amemhfiadhi bwana mkubwa ambaye ndiye aliyebebewa mzigo katika kashfa ya Richmond.

Sumaye pia alizungumzia madai kuwa Lowassa ni mgonjwa. Alisema mtu akishapita miaka 50 anapata matatizo ya maradhi.

Lakini hata kama mgonjwa, urais unahitaji kiongozi kuwa makini tu, kazi zinafanywa na timu nzuri anayoiteua. “Kazi hii anaiweza Mhe Lowassa.,” amesema.

Sumaye akasema kwamba kama Lowassa anasemwa na viongozi wa CCM kuwa ni mgonjwa, kwani hawajui kuwa Magufuli ni mgonjwa? Anakwenda Ulaya kila mwezi kufanya nini,” alihoji.

Taarifa za ndani ya serikali zinasema kwamba Magufuli amekuwa akienda kubadilisha damu Ulaya kutokana na kuugua ugonjwa mkubwa ulio maarufu. Hatua hiyo ya kubadilisha damu kila mwezi inagharimu fedha nyingi ambazo analipiwa na serikali anayoongoza Rais Kikwete.

Elimu – serikali itagharamia elimu ya watoto mpaka chuo kikuu. Inawezekana, tunapoteza mabilioni ya pesa kwa mambo yasokuwa na maana yoyote.

Kilimo – tutatanua uzalishaji na kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji. Mazao ya chakula wakulima wakikopwa, watalipwa na riba. Hakuna kuwanyonya wakulima wetu.

Reli ya Kati – itajengwa iende mpaka Kigoma.

Tutafufua Air Tanzania (ATC), nia ni pamoja na kuimarisha sekta ya utalii.

Nidhamu ya kazi muhimu.

Masheikh wa Zanzibar na Babu Seya – naelewa hisia zenu. Tutaona namna vya kuwatoa kifungoni.

Maji vijijini, Vyuo vya Ufundi.

Naomba kura, watakaonipatia kura wanyooshe mikono… watu wanasema hivi, kura tutapata nyingi lakini zitaibiwa. Kwa hivyo,” akasimamishwa kwa shangwe ya Rais, Rais, Rais.

“Rais peke yake haitoshi. Kura, kura, ni kuhakikisha mnakwenda kupiga kura. Wameniuliza nitafutieni kura kwa watu wa Bara. Hata wakiiba wataiba nyingi lakini zitabaki nyingi za kutosha,” amesema.

Lowassa amefurahishwa na mapokezi, akisema hata wakubwa zetu, hawajapata mapokezi haya.

error: Content is protected !!