Friday , 24 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sumaye awachonganisha CCM
Habari za Siasa

Sumaye awachonganisha CCM

Spread the love

BARAZA Kuu la Chadema Kanda ya Pwani kimetoa wito kwa serikali kuwachukulia hatua watu walioanzisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya au wanaokwamisha mchakato huo, likidai kuwa uamuzi huo umepoteza fedha za umma. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akitoa maazimio ya baraza hilo, leo tarehe 24 Desemba 2018 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye amesema kama mchakato huo ulioanzishwa na serikali ya CCM ya awamu ya nne haukuwa uamuzi sahihi, wahusika wachukuliwe hatua kwa ubadhirifu wa fedha za umma.

“Kama mchakato wa katiba ulioanzwa na serikali ya CCM ya awamu ya nne haukuwa uamuzi sahihi, wa serikali uliokuwa na Baraka za chama hicho tawala, sababu fedha zetu zimepoteza nyingi basi wahusika wachukuliwe hatua kwa ubadhirifu wa fedha za umma,” amesema Sumaye.

Katika hatua nyingine, Sumaye amesema kama mchakato huo ulikuwa halali na kupata baraka za CCM ,baraza hilo linaitaka CCM kuilazimisha serikali iliyopo madarakani kuuendeleza mchakato huo au kuwawajibisha wanaoukwamisha kwa kuwa fedha za umma zilizotumika katika mchakato huo zimepotea bila kuleta matokeo yaliyotarajiwa.

“Kama mchakato ulikuwa halali na wenye baraka za chama hicho tawala, basi watawala wa sasa ama chama chao kiwalazimishe kuendelea na mchakato wa katiba mpya au kiwashtaki na kuwawajibisha kwa ubadhirifu wa fedha za umma zilizopotea bila matokeo tarajiwa,” amesema Sumaye.

Sumaye ameeleza kuwa, kama mchakato huo ungefanikiwa, katiba mpya ingepatikana na kutoa mchakato mzuri kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko awataka makatibu mahsusi kujiendeleza, kuwa kielelezi cha huduma bora

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia muonee huruma Dk. Phissoo

Spread the loveRAIS wangu mama Samia, wiki iliyopita baada ya kuwa nimekuandikia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miaka 63 ya Uhuru bila katiba ya wananchi

Spread the loveWAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wanaharakati...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Serikali mbili ni sera ya CCM, si mkataba wa Muungano

Spread the loveMUUNGANO kati ya Tanganyika na Zanzibar uliotimiza miaka 60 tangu...

error: Content is protected !!