FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu, ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anaandika mwandishi wetu kutoka Dodoma.
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema – Taifa amekiambia Kikao cha Kamati Kuu jana kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho.
Amesema, dhamira ya Chadema ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila mwanachama kufanya kazi ya uenezi.
Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.
Naye Sumaye amemshukuru Mbowe kwa kumteuwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.
More Stories
Samia aungana na viongozi Afrika kumpongeza Ruto
Askari 818 wahitimu, wawili watimuliwa chuo cha uhamiaji
Dk. Makakala: Chuo cha uhamiaji chachu maendeleo, usalama