Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sumaye abwaga manyanga Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Sumaye abwaga manyanga Chadema

Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu
Spread the love

ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani, Fredrick Sumaye, ametangaza kukihama chama hicho.  Anaripoti Hamis Mguta … (endelea). 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo tarehe 4 Desemba, Sumaye alisema, ameamua amejiweka pembeni kwenye chama hicho, kwa manufaa ya usalama wake na familia yake.

Sumaye alitangaza kujiuzulu uwanachama wake huo na amekiri kusikia kauli tata kutoka mdomoni mwa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Amesema, “nimemsikia Mbowe, mwenyekiti wetu wa taifa alipokuwa mkoani Arusha kwenye mkutano wa uchaguzi wa Kanda ya Kaskazini. Alitutahadharisha, kwamba sumu haionjwi kwa ulimi, na mimi sina sababu ya kuonja sumu hiyo kwa ulimi.” 

Amesema, mazingira ndani ya chama hicho “yamemtisha” na kwamba ni bora kwake kukaa pembeni.

Dhoruba aliyokutana nayo Sumaye, kwa kuchokonoa nafasi ya uenyekiti wa Chadema taifa, imefanana na kile kilichowakuta Zitto Kabwe na Chacha Wangwe.

Kujiondoa kwa Sumaye ndani ya Chadema, kumekuja siku moja tangu Prof. Abdallah Safari, makamu mwenyekiti wa chama hicho (Bara), kukitaka chama chake, kuboresha “mfumo wa demokrasia.”

Aidha, kuondoka kwa Sumaye kumekuja wiki moja tangu kingozi huyo atangaze kugombea uenyekiti wa Mbowe.

Sumaye alirejesha fomu ya kuwania uenyekiti wa Chadema, tarehe 30 Novemba 2019. Alirejeshewa  fomu yake ya uenyekiti na Mustafa Muro, diwani wa Kata ya Kinondoni.

Mwanasiasa huyu alichukua maamuzi ya kurejesha fomu ya kuwania uenyekiti, siku mbili baada ya kuangushwa katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa Kanda ya Pwani.

Sumaye alishindwa katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani, baada ya kupigiwa kura nyingi za HAPANA.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wanamlaumu Sumaye kwa kushindwa kusoma alama za nyakati na historia ya waliojaribu kumgusa Mbowe, kwenye nafasi hiyo.

Mwaka 2018, Chacha Wangwe, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Bara, alitangaza kugombea uenyekiti wa Chadema. Aliong’olewa kwenye chama wake kwa tuhuma za usaliti.

Naye Zitto ambaye kwa sasa, ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, alitangaza kupima ubavu na Mbowe kwenye nafasi hiyo ya uenyekiti taifa mwaka 2009.

Katika video yake inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Zitto anahoji: “Mwaka 2009 nikasema, kwani kuna dhambi mtu wa Kigoma kuwa mwenyekiti wa chama (Chadema) taifa, kuna dhambi?”

Anahoji: “Nikagombea, hapo ndipo ilikuwa mwisho wa Amani yangu ndani ya chama,” alizungumza Zitto kwenye moja ya mikutano yake.”

Kwenye mkutano wake wa leo na waandishi wa habari, Sumaye amesema, “figisu za kuangushwa kwenye uchaguzi wa Kanda ya Pwani nilizijua mapema.”

Alisema, “hali hii ya kufanyiwa figisu ndani ya chama, niliijua mapema na akina nani walihusika. Kabla uchaguzi haujaanza, nilitahadhirsha wajumbe wa mkutano kwamba, mlichokipanga kwa kushawishiwa na wachache sio sahihi.

“Niliwambia Chadema inahushwa na kutokuwa na demokrasia ndani mwake, na kuwa kiti cha Mbowe hakiguswi. Niliwambia kama mtapiga kura kama mlivyopanga, basi mtaudhibitishia umma kuwa ni nafasi ya Mbowe haiguswi.”

Alihoji: “Huo ni uchaguzi gani ambao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu wanawaficha wajumbe na kuwalisha rushwa?… Walidhani wananikomoa mimi Sumaye, lakini wamekijengea chama mazingira ya hovyo na ya aibu.”

Akizungumza kwa sauti ya ukali, Sumaye alimuonya Mbowe na wale aliowaita ‘kabineti yake’ kujihadhari na makundi kwa kuwa kuendeleza tabia hiyo kutakivunja chama hicho.”

Sumaye aliyekuwa waziri mkuu kati ya mwaka 1995 hadi 2005. Aliondoka Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na upinzani Julai 2015, akisema alikusudia kuuimarisha upinzani na kuindoa CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!