October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sumatra wafanikiwa kumaliza tatizo la usafiri Ubungo

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) imefanikiwa kumaliza tatizo la usafiri wa abiria waoendao mikoani katika kituo cha mabasi cha Ubungo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Msongamano wa abiria umekwisha leo baada ya kuanzia jana Sumatra kuruhusu mabasi madogo aina ya Coaster yanayoichukua abiria 28 kubeba abiria kuelekea mikoani kutokea kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Udhibiti wa Barabara wa Sumatra, Johansen Kahatano amesema walilazimika kuruhusu mabao hayo  aina ya Coaster kuanza kusafirisha abiria baada ya mabasi ya kawaida kwisha huku idadi kubwa ya abiria ikihitaji usafiri kuelekea mikoani.

Kahatano amesema idadi kubwa ya abiria wakiwa wakielekea katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha ambao mpaka kufikia leo wamepingua kwa kiasi kikubwa kiasi cha mabasi ya kawaida kuweza kuwamudu, lakini abiria wanaoelekea mikoa ya Morogoro na Dodoma bado idadi yao ipo kubwa.

Amesema kwa sasa wanaelekeza nguvu zao kutatua tatizo la abiria wanaoelekea mikoa ya Morogoro na Dodoma ambapo wanaamini mpaka kufikia jioni tatizo hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi.

Pamoja na Sumatra kuondoa tatizo hilo lakini abiria wamelalamikia kutozwa nauli kubwa na magari hayo kwa madai yakienda yanarudi bila abiria.

Abiria wanaokwenda Moshi wamekuwa wakitozwa Sh30,000 badala ya Sh28,000 wakati na Arusha Sh35,000 badala ya Sh32,000.

error: Content is protected !!