March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sumatra waanzisha ruti ya kwenda Hospitali ya Mloganzila

Spread the love

MAMLAKA ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imetangaza ruti mpya za kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

SUMATRA imetangaza ruti hizo leo tarehe 24 Oktoba 2018 ambapo imearifu kuwa, kutakuwa na mizunguko miwili.

Ruti ya kwanza ni kutoka Kawe kwenda Mloganzila kupitia barabara ya Sam Nujoma na Morogoro ambayo itakuwa ni mzunguko wa kwanza.

Ruti ya pili ni kutoka Kawe kwenda Mloganzila kupitia barabara ya Goba na Bagamoyo, ikiwa ni Mzunguko wa pili.

Makumbusho kwenda Mloganzila kupitia barabara ya Bagamoyo na Sam Nujoma na Morogoro, ni ruti ya tatu mzunguko wa kwanza.

Wakati ruti ya nne ikiwa ni kutoka Makumbusho kwenda Mloganzila kupitia barabara ya Bagamoyo na Goba ikiwa ni mzunguko wa pili.

Ruti ya tano ni Mloganzila kwenda Tegetanyuki kupitia barabara za Goba, Madale na Wazo Hill ambayo ni mzunguko wa kwanza.

Kutoka Mloganzila kuelekea Tegetanyuki kupitia barabara za Goba, Masana Hospitali, na Bagamoyo ni ruti ya sita mzunguko wa pili.

Ruti ya mwisho ni kutoka Tabata Kimanga  kwenda Mloganzila kupitia barabara ya Maramba Mawili.

error: Content is protected !!