August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sumatra: Marufuku kupandisha nauli kiholela

Kituo cha mabasi Ubungo, Dar es Salaam.

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) imewataka wamiliki wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na madereva wao kuacha tabia ya kupandisha nauli katika kipindi hiki cha sikukuu, anaandika Christina Haule.

Kauli hiyo imetolewa na Joseph Burongo ofisa mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Morogoro, ambapo alieleza kuwa baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri wamekuwa na tabia ya kupandisha bei za nauli bila kufuata utaratibu uliopo.

“Kupandisha nauli hovyo ni kinyume cha utaratibu uliowekwa na mamlaka, fuateni viwango vilivyowekwa na mamlaka, atakayekamatwa akikiuka atachukuliwa sheria na kufikishwa mahakamani,” amesema Burongo.
Ameongeza kuwa, mpaka sasa hakuna mabadiliko yoyote ya kuongezeka au kupungua kwa nauli hivyo wamiliki wa vyombo vya usafiri wazingatie kiwango kilichopangwa na Sumatra, na kwamba wananchi waripoti iwapo watatozwa nauli tofauti.

“Hakuna mtu mwenye anayeruhusiwa kuvunja utaratibu na kupandisha nauli iliyopangwa na Sumatra kwahiyo tunawaomba wananchi watoe taarifa kwa mamlaka hiyo pindi watakapoona chombo chochote cha usafiri kinatoza kiwango tofauti cha nauli,” amesema.

Imekuwa ni utamaduni wa kawaida kwa wamiliki wa mabasi ya mikoani na madereva kupandisha nauli katika msimu wa sikukuu.

error: Content is protected !!