October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sukari Morogoro majanga, wafanyabiashara wasusa

Wananchi wakiwa katika msongamano wa kununua sukari

Spread the love

UPATIKANAJI wa sukari katika Mkoa wa Morogoro, umekuwa mgumu kutokana na uhaba unaotajwa kuchagizwa na bei elekezi ya serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Taarifa kutoka Morogoro zinaeleza, leo tarehe 10 Mei 2020, kilo moja ya sukari inauzwa kati ya Sh. 5,000 na 7,000 na kwamba, haipatikani katika maduka mengi ya rejareja.

“Ukienda kununua katika maduka ya whole sale (duka la jumla) unakuta bei kubwa tofauti na serikali inavyotuambia.

“Kwa hiyo tunaogopa kuchukua kutokana na kwamba tutapochukua, tutakuja kukamatwa. Hatukutaka kuchukua kwa kuwa tunauziwa mpaka laki na nusu (kwa kilo 100),” amesema Suleiman Rashid ambaye ni mfanyabiashara kwenye Manispaa ya Morogoro.

Baadhi ya mama lishe mkoani humo wamesimamisha baadhi ya huduma, ikiwemo chai kwa kuwa, bei yake haiwezi kukidhi kutokana na sukari kupanda bei.

Awananchi wamelalamika kwamba, licha ya sukari kuwa na bei kubwa, bado haipo kwenye maduka mengi hivyo kulasimika kuisaka katika maeneo mbalimbali

“Bora sukari ingekuwa hata inapatikana kwenye maduka, lakini kwa sasa haipo,” amesema mwananchi mmoja na kuongeza “serikali tunaomba iingilie kati suala hili.”

Regina Chonjo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro amesema, amewataka wafanyabiashara wa wilaya hiyo kutojipangia bei na kusisitiza wafuate bei ya serikali.

error: Content is protected !!