May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

SUK ni ‘sherehe’ Z’bar

Jaji Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Omar Othman Makungu

Spread the love

UAMUZI wa Chama cha ACT-Wazalendo kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani Zanzibar (SUK), unaonekana kuwa wa busara. Anaandika Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Serikali ya Zanzibar inaundwa na vyama viwili – Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ACT – Wazalendo, ambacho kimetoa Makamu wa Kwanza wa Rais kwenye serikali hiyo, Maalim Seif Sharif Hamad.

Kutokana na ACT-Wazalendo kuridhia kuingia kwenye serikali na kufanikiwa muundao wa SUK, Omari Othuman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar amesema ‘serikali sasa ni ya weledi na kasi.’

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Alitoa kauli hiyo jana Alhamisi tarehe 7 Januari 2021, wakati akiwasilisha salamu za Zanzibar kwenye Mkutano wa 10 wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).

“Wananchi, serikali, viongozi wa vyama vya siasa wote kwa sasa tunazungumza lugha moja,” alisema na kuongeza “muiunge mkono Serikali ya awamu ya nane Zanzibar kukabiliana na changamoto za kisheria.”

Jaji Makungu anakuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu Zanzibar kueleza hisia zake kuhusu muungano huo akitanguliwa na Abeid Aman Karume, Rais Mstaafu visiwani humo.

Rais Karume alisema, kilichoonekana kwa sasa kabla ya (ACT-Wazaelendo) kuingia serikalini, ni matokeo ya kukosekana kwa upinzani.

Aman Abeid Karume, Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

“Kinachoonekana sasa ndani ya Serikali ya Zanzibar, kwa kiasi kikubwa, msingi wake mkuu, ni kutokuwapo kwa uwakilishi wa upinzani kwenye Baraza la Wawakilishi na serikalini katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

“Malalamiko ya sasa juu ya kuwapo kwa madai ya ufisadi, ubadhilifu na wizi wa fedha za Serikali Visiwani Zanzibar, kwa kiasi kikubwa, yanatokana na kukosekana kwa upinzani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.”

Alisema, kukosekana kwa wawakilishi wa vyama vya upinzani bungeni na Baraza la Wawakilishi, kunachochea Serikali kuwa dhaifu kusimamia kazi zake.

Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kuvurugwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza marudio, kilichokuwa chama kikuu cha upinzani visiwani humo – Chama Cha Wananchi (CUF) – kilipinga hatua hiyo, jambo lililosababisha kuwepo nje ya SUK chini ya uongozi wa aliyekuwa rasi, Dk. Ali Mohamed Shein.

error: Content is protected !!