July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sugu: Serikali isiniite tena kutuliza fujo Mbeya

Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha

Spread the love

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) ametoa angalizo kwa Serikali, akiitaka itatue mgogoro wa wafanyabiashara mkoani humo, vinginevyo asiitwe tena kuwatuliza pale hali itakapokuwa mbaya. Anaadika Mwandishi Wetu … (endelea).

Mbilinyi maarufu kama Sugu, alitoa angalizo hilo leo asubuhi bungeni wakati akiomba mwongozo kwa Spika Anne Makinda, akimtaka aishauri serikali itoe kauli ya kumaliza mgogoro baina ya wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhusu matumizi ya mashine za elektroniki.

“Mheshimiwa Spika hali ya Mbeya ni mbaya, wafanyabiashara wamefunga maduka yao tangu juzi mpaka leo, wananchi wanakosa huduma na serikali haitatui mgogoro huo.

“Hivi kama shida ni huyo kiongozi wao Minja (Johnson) aliyewekwa ndani, nikwanini asipewe dhamana halafu wakakaa na serikali na kumaliza mgogoro huo. Kwani amefanya kosa gani lisilodhaminika, ameua au amebaka? Alihoji Sugu.

Hata hivyo Sugu alimejikuta akiingia katika majibizano ya kauli na Spika wakati akijenga hoja yake pale alipodai anaingiliwa badala ya kuachwa  amalize kusema.

Amesema “kama serikali haitakaa na wafanyabiashara na kutatua mgogoro huu Mbeya, safari hii msiniite tena kuja kutuliza vurugu zitakapotokea kama mlivyofanya kwenye vurugu zilizopita”

error: Content is protected !!