ALIYEKUWA kuwa Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujasiri wa kuondoa zuio haramu la mikutano ya hadhara lililodumu zaidi ya miaka saba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).
Pia amesema si kweli kwamba vyama vya upinzani havina ajenda bali ajenda zipo za kutosha hasa ikizingatiwa bidhaa nyingi za chakula zimepanda bei.
Sugu ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Januari, 2023 wakati akisalimia wananchi katika uzinduzi rasmi wa mikutano ya hadhara kwa Chadema mkoani Mwanza.
“Wanasema hatuna hoja sasa tunaenda kuwaonesha kwamba tuna hoja. Kama tunavyoona hali ni tete, wananchi wamechoka kupitia mikutano ya hadhara tunaenda nchi nzima kuwaeleza wananchi kuhusu tozo na kodi zilizo mizigo kwa wananchi.
“Mkoani Mbeya katika kipindi cha miezi sita iliyopita debe moja la mchele ilikuwa 28,000 leo ni 64,000… wanasema hatuna hoja! wakae kwa kutulia na mikutano ndio hii,” amesema Sugu na kushangiliwa kwa wingi na wananchi waliofurika kwenye mkutano huo.
Leave a comment