August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sugu: Kifo hiki kimeniumiza, nisameheni

Joseph Mbilinyi (Sugu), Mbunge wa Mbeya Mjini

Spread the love

SIKU moja baada ya gari la Joseph Mbilinyi (Sugu), Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chadema kumgonga Recho Lutumo (14) na kumuua, mbunge huyo ameomba radhi familia ya marehemu, anaandika Mwandishi Wetu.

Ajali hiyo ilitokea katika Barabara Kuu ya Zambia kwenye eneo la Iyunga ambapo Neema alikuwa akivuka kwenye kivuko cha waenda kwa miguu.

Gari la Sugu lilikuwa likiendeshwa na Gabriel Andrew (43) akitokea jijini humo kwenda katika Uwanja wa Ndege wa Songwe (SIA).

Wakati wa maandalizi ya maziko ya Neemba akiwa pamoja na ndugu wa marehemu, mbunge huyo alieleza masikitiko yake ya kumpoteza binti kwenye ajali hiyo.

Sugu amesema moja ya matukio mabaya kutokea akiwa mbunge ni la kupoteza Neema ambaye ni mkazi wa Mbeya na raia wa Mtanzania.

“Naomba mnisamehe. Kifo hiki kimeniumiza, nawaomba radhi ndugu wanafamilia na wananchi wa Mbeya,” ameeleza Sugu kwenye msiba huo.

Dhahiri Kidavashari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya amesema Gabriel ambaye ni dereva wa Sugu, anashikiliwa na jeshi hilo.

error: Content is protected !!