Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Sugu ataka wateule wa JPM wachunguzwe kwa ufisadi, amtumia salamu Spika Tulia
Habari za Siasa

Sugu ataka wateule wa JPM wachunguzwe kwa ufisadi, amtumia salamu Spika Tulia

Joseph Mbilinyi 'Sugu'
Spread the love

 

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, ameshauri baadhi ya wateule wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli, wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wachunguzwe ili mali walizojilimbikizia zirudishwe serikalini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Sugu ametoa wito huo jana tarehe 1 Machi 2023, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Chadema, uliofanyika jijini Arusha.

Mwanasiasa huyo aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chadema, alidai kuna baadhi ya waliokuwa mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya katika uongozi wa awamu hiyo, walikuwa wanafanya ufisadi.

“Wanasema awamu ya tano ilizuia ufisadi lakini hakuna awamu iliyokuwa na ufisadi kwa wazi mpaka ngazi ya wakuu wa mikoa kama awamu ya Magufuli na walikuwa wana ukwasi wa hali ya juu, wananyang’anya mali za watu wanajenga nyumba, wanafanya kila kitu wakati mishahara yao ilikuwa Sh. 2 milioni,” alidai Sugu.

Sugu alidai “watu walifanya ufisadi sana haina namna wanatakiwa wachunguzwe ili mali walizoiba kwa umma zirudi kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, Sugu amemtaka mrithi wake katika Jimbo la Mbeya Mjini, ambaye ni Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, ajiandae kung’oka katika uchaguzi mkuu ujao wa 2025.

“Hii ni salamu kwamba sababu ya mwendazake ndiyo imekuwa hivi, bila mwendazake sio yeye wala dada ake wa Mbeya watakaokwenda kutoboa. Hata uchaguzi ukifanyika kesho asubuhi hawawezi kutoboa,” alisema Sugu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!