ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, amesema umefika wakati kila raia amiliki ardhi yake badala ya Rais kupewa mamlaka ya kusimamia ardhi yote nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Musoma…(endelea)
Mbilinyi ameyasema hayo leo Jumapili tarehe 22 Januari, 2023 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Musoma ikiwa ni mwendeleoz wa uzinduzi wa mikutano ya siasa iliyokuwa imezuiliwa tangu kipindi cha Serikali ya awamu ya tano.
Mjumbe huyo wa Kamti Kuu ya Chadema amesema ardhi ndiyo chanzo cha utajiri wote duunniani hivyo ni lazima imilikiwe na raia ili waweze kujikwamua na umasikini.
“Rais asiwe custodian (msimamizi) wa ardhi, yaani bongo wanasema ardhi yote ni mali ya Rais yaani wewe hati yako inapewa miaka 33 ikifika miaka 33 Rais anaamua uendelee ama usiendelee sasa hii sio sawasawa sana, kila raia anapaswa amiliki ardhi yake,” amesema Mbilinyi.
Katika hatua nyingine amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake ya kuondoa mambo ya “hovyo” yaliyokuwepo awali.
“Tumetoka katika hali ngumu sana, miaka saba bila siasa na mateso mengine mengi, wanasiasa tulifungwa hovyo, wafanyabiashara walifilisiwa hovyo na kunyang’anywa fedha zao.
“Kwa tunakoelekea sasa tunaweza kumpongeza Rais Samia kwa hatua aliyofikia ya kuondoa yale mambo ya hovyo yote,” amesema Mbilinyi.
Leave a comment