March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sugu alisimamisha Bunge kwa muda

Joseph Mbilinyi 'Sugu' Mbunge wa Mbeya Mjini

Spread the love

KISHINDO cha Joseph Mbilinyi (Sugu) Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), kimesimamisha shughuli za Bunge kwa muda wa takribani dakika sita ikiwa ni mapokezi yake ndani ya bunge kwa mara ya kwanza tangu atoke gerezani. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Sugu aliiachiwa huru kutoka magereza Mei 10, mwaka huu kwa msamaha wa Rais John Magufuli. Leo kwa mara ya kwanza ameingia bungeni akiwa na mbunge Viti Maalum Kuntu Yusuph (Chadema).

Wabunge wa upinzani walisherehekea ujio wa Mbunge huyo huku wakigonga meza kwa furaha wakimshangilia kwa kishindo cha dakika tatu.

Wakati huo, Naibu Waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege aliyekuwa anajibu maswali ya wabunge, alikaa kimya kwa muda kupisha mapokezi ya mbunge huyo.

Alitinga na suti nyeusi ambapo upande wa kushoto kuna nembo inayoonyesha namba ya mfungwa yenye taarifa za kifungo alichotumikia.

Sugu aliingia ndani na kuanza kuwasilimia wabunge kwa kuwa mikono aliianza kwa Nape Nnauye Mbunge wa Mbunge wa Mtama, Dk. Adelardus Kilangi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika akawapa na kumpa mkono kisha kwa Jenister Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu.

Sugu alielekea upande walioketi wabunge wa upinzani na kukumbatiana na mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini na kwenda kukaa sehemu yake karibu na mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko.

Andrew Chenge, Mwenyekiti wa Bunge aliwaomba wabunge kutulia ili shughuli za Bunge ziendelee, huku akiwatishia kuwa hatawapa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza.

“Imetosha sasa, imetosha, haya endelea,” amesema Chenge.

error: Content is protected !!