December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sugu aeleza aibu ya Uwanja wa Ndege Mbeya

Uwanja wa Ndege wa Songwe

Spread the love

KIPINDI ambacho Uwanja wa Ndege wa Songwe, Mbeya unapogubikwa na ukungu, rubani hupata tabu kutua na wakati mwingine hulazimika hurudisha ndege Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ndege hushindwa kutua kutokana na kutokuwepo kwa taa hizo ambazo ni utaratibu wa kawaida kuwepo kwenye viwanja vyote. Kukosekana kwake husababisha kuvuruga ratiba za abiria pale wanaposhindwa kufika eneo husika kwa wakati kipindi cha ukungu.

Joseph Mbilinyi (Sugu), Mbunge wa Mbeya Mjini, ameihoji serikali lini itafanya marekebisho katika uwanja huo ili kuondoa na usumbufu unaowakabili wasafiri.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo tarehe 4 Februari 2019, Sugu amesema, aliwahi kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya mara mbili bila ndege kutua kwenye uwanja huo na matokeo yake kurudishwa Dar es Salaam kutokana na wanjanja huo kutokua na taa za kusaidia marubani wakati wa ukungu.

“Lini ujenzi wa jengo la abiria utakamilika kwenye Uwanja wa Songwe, Mbeya? Sasa hivi kukiwa na ukungu na hakuna taa, rubani hatui.

“Mimi mwenyewe nimerudi Dar mara mbili kutokana na ndege kushindwa kutua sababu ya ukungu,” amesema Sugu.

Akijibu swali la Sugu, Mhandisi Isaack Kamwele, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi amesema, tayari serikali imetangaza tenda ya ujenzi wa uwanja huo hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.

error: Content is protected !!