August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

SUA yafurahia mafanikio

Spread the love

CHUO Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kimefanikiwa kuboresha thamani ya mazao kwa wakulima, wafugaji na watunza mazingira kupitia miradi 17 kwenye mikoa 12, wilaya 22, vijiji 127 na kaya 4,151 nchini, anaandika Christina Raphael.

Profesa Lusato Kurwijila, Mratibu wa Programu ya Miradi ya Utafiti (EPINAV) amesema hayo leo kwenye kongamano la tatu na la mwisho la programu hiyo lililofanyika Morogoro.

Programu hiyo ina lenga kuboresha ubunifu kwa kuunganisha wakulima na watendaji wa ofisi za wakuu wa wilaya, mpango ujulikanao kama mnyororo wa thamani kwa mazao ya kilimo na maliasili.

Almesema kuwa, kufuatia ushirikishwaji huo wa watendaji wa wilaya hasa wakurugenzi wa wilaya, teknolojia zilizotafitiwa zimeweza kumfikia mkulima na kufanya kupata mazao bora na kuuza kwa thamani na hatimaye kujikwamua kiuchumi.

“Tumeweza kumsaidia mfugaji wa mbuzi wa maziwa, ng’ombe, nyuki, misitu na hata samaki, wote wameboresha mazao yao na kuweza kupata faida maradufu zinazoweza kuwasaidia kukuza uchumi,” amesema Prof. Kurwijila.

Prof. Kurwijila amesema, EPINAV imeweza kuwafikia wadau mbalimbali wa kilimo na biashara kwa kuboresha usindikaji na utoaji huduma za pembejeo za kilimo.

Awali akifungua kongamano hilo Prof. Susan Msolla, Mkuu wa SUA amewataka watafiti na wakulima walioshiriki katika miradi ya EPINAV kutumia kwa vitendo majadiliano waliyoyapata kwenye kongamano hilo ili kuinua kipato cha wananchi na kuleta maendeleo ya nchi.

error: Content is protected !!