June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

SUA kutumia teknolojia kupambana na magonjwa

Spread the love

CHUO Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), kimeanzisha Ndaki mpya (College), ya Sayansi ya Tiba za Wanyama na Binadamu kitakachotumia teknolojia ya mawasiliano kutoka kwa jamii hadi kwenye wizara husika jambo litakalosaidia kudhibiti magonjwa hayo kwa haraka, anaandika Christina Haule.

Prof. Patrick Mwang’ingo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo taaluma-SUA, amesema kisayansi kuna mahusiano makubwa kati ya binadamu na wanyama na kwamba kuanzishwa kwa chuo hicho kutasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu katika mikoa ya Morogoro na Dar es salaam.

“Tutashirikiana na taasisi ya Taifa ya utafiti wa wa magonjwa ya binadamu NIMR, tutaweza kudhibiti magonjwa mengi yatakayojitokeza na kuzuia athari zake, ikiwemo vifo vya binadamu na wanyama, amesema.

Tangu mwezi Agosti mwaka 2015, Tanzania ilikuwa ikikabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu ambao uliripotiwa kutoka katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo hadi mwezi Septemba, 2016 jumla ya kesi 22,595 ziliripotiwa sawa na asilimia 1.5.

“Tumetengeneza nyenzo za Tehama kwa kutumia simu za mkononi za kisasa ili kutoa taarifa za magonjwa kwa mnyama na binadamu ili kuifikia wizara ya Afya kiurahisi,” amesema Prof. Esron Karimuribo, mkuu wa mradi huo.
Ndaki hiyo ni ya kwanza na ya kipekee kuwepo hapa nchini na Afrika kwa ujumla ambapo watafiti kutoka katika nchi za Zambia, Kenya, Malawi, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania wameweza kushiriki na kujadili juu ya muendelezo wa mapambano ya magonjwa hayo katika nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika.

error: Content is protected !!