Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu SUA kuhakikisha tafiti zinazofanywa zisiachwe kwenye makabati
Elimu

SUA kuhakikisha tafiti zinazofanywa zisiachwe kwenye makabati

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Japhet Kashaigili
Spread the love

 

MRATIBU wa utafiti na machapisho katika kurugenzi ya uzamiri, utafiti wa urushaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalam kutoka Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Japhet Kashaigili amesema SUA inakusudia kusimamia tafiti zinazofanywa na kuachwa kabatini zitumike kwa kuhakikisha matokeo yake yanawafikia walaji. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Prof. Kashaigiri alisema hayo jana kwenye Kongamano la kisayansi la siku mbili katika wiki ya kumbukizi ya 18 ya Hayati Edward Moringe Sokoine lililoandaliwa na SUA na kufanyika chuoni hapo.

Alisema tafiti nyingi za kisayansi zimekuwa zikifanyika na kuishia kubaki makabatini jambo ambalo sio dhamira halisi ya tafiti kutoka kwenye taasisi husika.

Prof. Kashaigili alisema tafiti zinazofanya hutumia fedha nyingi kwa ajili ya kuongeza uelewa, kutatua matatizo mbalimbali na zingine ni kwa ajili ya kutafuta matokeo ya awali katika kutatua changamoto mbalimbali za nchi katika kuleta maendeleo.

Hata hivyo alisema zipo modeli mbalimbali za kisayansi zinazoweza kusaidia kurudisha uoto wa asili ikiwemo viashiria kwenye program za kompyuta katika kutambua kwa kuonesha kitu gani kinatokea wapi na kwa wakati gani na kusaidia kukabiliana na changamoto zake sambamba na mabadiliko ya tabianchi yanayoletwa na shughuli za kibinadamu.

Hivyo aliishauri jamii kuendelea kufanya shughuli mbalimbali huku wakitambua kuwa mazingira yanapaswa kutunzwa sababu wakiyaharibu leo na kesho wanaathirika wao wenyewe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

error: Content is protected !!